1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRASBOURGH.Ripoti inayoshutumu nchi kadhaa ya umoja wa ulaya yaidhinishwa

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCS5

Bunge la umoja wa ulaya limeidhinisha ripoti inayo shutumu nchi kadhaa za umoja wa ulaya kwa kufumbia macho shughuli za kisiri za shirika la ujasusi la Marekani CIA.

Inadaiwa kwamba shirika la CIA liliwazuilia kisiri washukiwa wa ugaidi barani ulaya na kuwasafirisha kwa ndege katika mataifa yanayoruhusu vitendo vya mateso dhidi ya mahabusu.

Katika ripoti hiyo serikali za nchi 10 wanachama wa umoja wa ulaya ikiwemo Ujerumani, Uingereza, Poland na Uhispania zimelaumiwa kwa kunyamaa kimya aidha kujua kuhusu kusafirishwa kwa siri washukiwa wa ugaidi au nchi hizo kutumika kama vituo vya safari za ndege za shirika la ujasusi la Marekani CIA.

Madai ya baadhi ya nchi za umoja wa ulaya kusema kwamba hazikujuwa kilichokuwa kinaendelea hayakupewa umuhimu.

Ripotri hiyo imetaja kuwa zaidi ya safari za ndege 1,200 ambazo hazikuorodheshwa zilifanywa na shirika hilo la ujasusi la CIA katika anga za umoja wa ulaya tangu kufanyika shambulio la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani.