1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Strasboug. Bunge la Ulaya lamtaka Wolfowitz kujiuzulu.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC70

Bunge la umoja wa Ulaya limetoa wito kwa rais wa benki kuu ya dunia Paul Wolfowitz kujiuzulu.

Bunge hilo lililoko katika mji wa Strasbourg , limepitisha azimio hilo kwa kura 333 dhidi ya 251.

Huu ni wito wa hivi karibuni kabisa wa kujiuzulu Wolfowitz kutokana na madai kuwa alionyesha upendeleo kwa kupanga kupandishwa cheo na mshahara kwa mpenzi wake wa kike.

Jopo maalum linachunguza iwapo Wolfowitz alikwenda kinyume na sheria za benki hiyo katika kushughulikia upandishaji cheo wa Shaha Riza kwenda katika kazi yenye mshahara wa juu katika wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani mwaka 2005