1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STOCKHOLM : Ertl ashinda tuzo ya Nobel ya Kemia

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gu

Gerhard Ertl amejishindia Tuzo ya Nobel ya Kemia ya mwaka 2007 kwa utafiti wake wa michakato ya kemikali kwa mahala pagumu.

Taasisi ya Taaluma ya Sayansi nchini Sweden imesema utafiti wake umesaidia kufahamu vipi vichocheo vinavyoweza kufanya kazi kwenye magari,betri za nishati zinavyofanya kazi na hata jinsi chuma kinavyoshika kutu.Ertl ambaye ametimiza miaka 71 leo hii alikuwa ameemewa mno na furaha kwa kutuzwa tuzo hiyo. Hii ni tuzo ya pili ya Nobel kuzawadiwa Ujerumani mwaka huu baada ya Peter Grunberg hapo Jumanne kujishindia tuzo ya phizikia.

Tuzo za Nobel huwa zinatolewa kila mwaka kwa mafanikio katika sayansi,fasihi,uchumi na amani.