STOCKHOLM : Bastola yahusishwa na mauaji ya Palme | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

STOCKHOLM : Bastola yahusishwa na mauaji ya Palme

Polisi ya Sweden imegunduwa bastola inayohusishwa na mauaji ya Waziri Mkuu Olof Palme hapo mwaka 1986.

Bastola hiyo imepatikana kwenye ziwa katikati ya Sweden hata hivyo polisi imesema ni mapema mno kusema iwapo hiyo ndio ilikuwa silaha halisi ya mauaji ambayo imepelekwa kufanyiwa uchunguzi kwenye maabara.Afisa alieko kwenye timu ya uchunguzi huo amesema uchunguzi umeonyesha kwamba risasi kutoka kwenye bastola hiyo ambayo ilitumiwa kwa ajili ya wizi hapo mwaka 1983 inafanana na zile zilizopatikana katika eneo la mauaji ya Palme.

Mauaji ya kiongozi huyo wa Sweden hadi leo yamekuwa kitendawili ambapo sio muuaji wala silaha iliotumika kwa mauaji hayo vimeweza kupatikana katika uchunguzi unaoendelea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com