1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPD yakanusha kujiuzulu kwa Gabriel

8 Mei 2016

Naibu mwenyekiti wa chama cha SPD mshirika katika seikajli ya mseto nchini Ujerumani Ralf Stegner amepuuzilia mbali repoti za kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama hicho Sigmar Gabriel.

https://p.dw.com/p/1Ik2t
Picha: Getty Images/C. Koall

Kukanushwa huko Jumapili (08.05.2016) kumekuja masaa machache baada ya mhariri wa kijarida cha habari nchini Ujerumani cha "Focus" Helmut Markwort kudai kwenye televisheni ya Bavaria kwamba amepata habari kutoka duru za kuaminika kwamba mwenyekiti huyo wa chama cha SPD Sigmar Gabriel alikuwa anataka kujiuzulu.

Markwort alisema Olaf Scholz meya wa mji wa Hamburg atakuwa mwenyekiti mpya wa SPD na Martin Schulz wa bunge la Ulaya yuko katika mazungumzo ya kuwa mgombea mkuu wa Ukansela.

Hata hivyo Stenger amemdhihaki Markwort Jumapili hii kwa kuandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba yumkini mwandishi huyo jua kali mno lilimpata huko Munich.

Stegner ameongeza kusema yoyote yule aliekuwa na duru hizo nzuri atakuwa ameboronga.Wanachama wengine wa SPD pia wamesema madai hayo ni upuuzi..

Wazir wa Sheria Heiko Maas amesema katika kipindi cha "Bericht aus Berlin" yaani "Baruwa kutoka Berlin" kilichorushwa na kituo cha ARD kwamba "ni upuuzi mtupu ambao hauhitaji hata kukanushwa."

Kinachomsibu Gabriel

Uvumi huo kwenye mtandao umekuja hapo Jumapili wakati gazeti mashuhuri la Ujerumani la "Bild am Sonntag "" likiripoti kwamba Gabriel alikuwa anauguwa ugonjwa wa vipele ikiwa ni matokeo ya msongo wa mawazo.Naibu kansela huyo ambaye ni waziri wa uchumi pia amefuta ziara yake iliokuwa imepangwa kwenda Iran miwshoni mwa juma lililopita na hiyo kuzidisha tetesi ndani ya chama chake cha SPD kuhusu afya yake.

Sigmar Gabriel Mwenyekiti wa SPD.
Sigmar Gabriel Mwenyekiti wa SPD.Picha: Imago/CommonLens

Gazeti hilo pia limeripoti hapo Jumapili kwamba Gabriel alikuwa anapanga kuahirishwa kutangazwa na chama hicho kwa mgombea mkuu wa chama katika uchaguzi mkuu wa mwakani hadi mwezi wa Mei badala ya mapema mwakani.

Gazeti hilo la Bild am Sonntag likimkariri afisa wa ngazi ya juu wa chama cha SPD limesema kucheleweshwa huko kutakiwezesha chama hicho kufanya tathimini ya uchaguzi wa mwakani wa majimbo kwa jimbo la North Rhine- Westphalia jimbo lenye idadi kubwa kabisa ya watu nchini Ujerumani kabla ya kuamuwa iwapo ifanye mabadiliko makubwa ya uongozi.

Umashuhuri wa SPD washuka

Chama hicho kimefanya vibaya sana katika uchaguzi wa majimbo hapo mwezi wa Machi wakati kilipopitwa na hata chama kichanga cha sera kali za mrengo wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani (AfD) katika majimbo mawili kati ya matatu.

Viongozi wa SPD.
Viongozi wa SPD.Picha: picture-alliance/dpa/W. Kumm

Uchunguzi wa mwisho wa maoni wa kijarida cha Star umeonyesha chama hicho kikiungwa mkono kwa asilimia 21 kikitanguliwa na chama cha Angela Merkel cha CDU kikiwa na asilimia 34.

Uvumi umekuwa ukizagaa ju ya nani atachaguliwa kuwa mgombea mkuu wa chama cha SPD katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.Alipoulizwa hapo mwezi wa Machi iwapo mweyewe binafsi atagombania ukansela Gabriel alisema : " Tutaamuwa walati utakapofika. "

Mwandishi : Mohamed Dahman /Reuters/dpa /AFP

Mhariri : Yusra Buwayhid