1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPD kujadili chama cha Left

10 Machi 2008

Kamati kuu ya taifa ya chama cha Social Demokartic nchini Ujerumani leo inatazamiwa kukutana mjini Berlin kujaribu kukubaliana juu ya namna ya kukishughulikia chama cha Left cha sera aza mrengo wa shoto.

https://p.dw.com/p/DLXk

BERLIN

Chama cha SPD kimekuwa kwenye machafuko kutokana na mpango wa kiongozi wake kwenye jimbo la Hesse wa kuunda serikali kwa kuungwa mkono kimya kimya na chama hicho ambacho kinaundwa na makomunisti wa zamani wa Ujerumani mashariki na wanachama wa zamani wa kitengo cha mrengo wa shoto wa chama cha SPD.Andrea Ypsilanti alilazimishwa kuachana na mpango huo wiki iliopita baada ya mbunge mmoja wa SPD katika bunge la jimbo hilo la Hesse kusema kwamba hatompigia kura ya uwaziri mkuu wa jimbo hilo kwa sababu amekengeuka ahadi yake ya kutoshirikiana na chama hicho cha mrengo wa shoto.

Kiongozi wa taifa wa chama cha SPD Kurt Beck hapo awali aliunga mkono mpango huo lakini wabunge waandamizi wa chama cha SPD hivi sasa wanasema mama huyo Ypsilanti alichukuwa hatua hiyo peke yake.

Haiko wazi iwapo mama huyo atajaribu upya kuunda serikali hiyo.