1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia kufanya mkutano wa maridhiano.

Sekione Kitojo15 Machi 2007

Waziri mkuu wa serikali ya mpito nchini Somalia Ali Mohammed Gedi ametoa wito Jumatano wiki hii wa nchi yake kupatiwa kiasi cha dola milioni 42 ili kuweza kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu, ili kuitisha mkutano wa maridhiano katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

https://p.dw.com/p/CHI8

Nachukua nafasi hii kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa , washirika na marafiki wa Somalia kusaidia juhudi zetu kuelekea kufanikiwa maridhiano ya kweli, utawala bora na amani ya kudumu nchini Somalia, Ali Mohammed Gedi amesema wakati akihutubia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ambako alikutana hapo kabla na wawakilishi wa mataifa fadhili.

Mkutano wa kitaifa wa maridhiano unatarajiwa kuwakutanisha pamoja kiasi cha Wasomali 3,000 kutoka sehemu mbali mbali, ikiwa ni pamoja na koo na viongozi wa makundi, wanasiasa , wafanyabiashara, wawakilishi wa jumiya za kidini, na raia wanaoishi nje ya nchi hiyo.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika hapo Aprili 16 mjini Mogadishu na utafanyika kwa muda wa miezi miwili, ambapo wajumbe watatoa maelezo kuhusu kutendewa vibaya Wasomalia wakati wa mzozo ambao umeanza mwaka 1991 baada ya kuangushwa kutoka madarakani dikteta Mahammed Siad Barre.

Maridhiano ya kijamii ni muhimu ili kuponya majeraha yaliyosababishwa na machafuko ya kijamii ili kuweza kusafisha njia kuelekea ujenzi mpya na maendeleo ya Somalia, Gedi amedokeza.

Maneno haya yamesemwa pia na Mohammed Abdi Hayir, waziri anayehusika na maridhiano. Tunahakika kuwa amani ya kudumu itakuja kutokana na mkutano huu. Tunamatarajio makubwa kwa mkutano huu, kwasababu tunafahamu kuwa utabadilisha hali ya Somalia, ameliambia shirika la habari la IPS.

Kuanguka kwa utawala wa Siad Barre kulifungua mlango wa mivutano ya makundi mbali mbali hali iliyosababisha mamia kwa maelfu ya vifo pamoja na watu wengi zaidi kukimbia makaazi yao, wakati Wasomali waliingia kipindi ambacho kwa muda mrefu hawakuwa na serikali.

Juhudi kadha za kurejesha hali ya utulivu nchini humo ilifuatiwa na uundwaji wa serikali ya mpito mwaka 2004. Hata hivyo hali ya kutokuwa na amani imeilazimisha serikali mpya ya mpito kuweka mamlaka yake katika mji wa Baidoa badala ya mji mkuu Mogadishu, na pia kuzuwia maafisa wa serikali ya mpito kuweza kupanua mamlaka yao kupindukia maeneo ya mji huo wa kusini.

Katikati ya mwaka 2006 umoja wa mahakama za Kiislamu UIC ulifanikiwa kile ambacho serikali ya muda haikuweza, kuchukua udhibiti wa mji mkuu na maeneo makubwa ya eneo la kusini mwa Somalia. Umoja huo wa UIC ulipinduliwa na majeshi ya serikali ya mpito yakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia katika kampeni ambayo ilianza mwishoni mwa mwaka jana, na jeshi la kulinda amani la umoja wa Afrika linawekwa hivi sasa nchini Somalia.

Lakini Mogadishu uko bado katika mikono ya ghasia zinazozidi.

Rais Abdulahi Yusuf aliingia mjini Mogadishu siku ya Jumanne, siku moja ya bunge kupiga kura kuidhinisha serikali yote kufanyakazi zake mjini humo, lakini makao yake yalishambuliwa katika shambulio la makombora ambalo lilifanyika saa chache baada ya kuwasili. Wakati serikali inasema kuwa watu wawili wameuwawa, lakini wakaazi wa eneo hilo wanadai kuwa waliouwawa wanafikia 15.

Majeshi ya serikali ya mpito na yale ya Ethiopia mjini Mogadishu yameripotiwa kushambuliwa na wapiganaji. Wasomalia wengi hawajisikii vizuri wawaonapo wanajeshi wa Ethiopia, ambayo ina historia ya uhusiano wa wasi wasi na Somalia.

Ndege iliyokuwa imebeba wanajeshi wa Uganda wa jeshi la kulinda amani la umoja wa Afrika pia inasemekana ilishambuliwa wiki iliyopita, na ndege hiyo kushika moto wakati ikijitayarisha kutua katika mji mkuu Mogadishu.

Ghasia hizo zimeanza kuathiri hata watu ambao haw