SOFIA:Bush akamilisha ziara barani Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 11.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SOFIA:Bush akamilisha ziara barani Ulaya

Rais George Bush wa Marekani yuko ziarani katika mji mkuu wa Bulgaria wa Sofia.Kiongozi huyo amefikia mkondo wa mwisho wa ziara yake ya bara la Ulaya.Mazungumzo kati yake na viongozi wa Bulgaria yanatarajiwa kujadilia mpango wake wa kuweka makombora ya kujihami Ulaya mashariki vilevile mustakabal wa jimbo la Kosovo.

Mapema Rais Bush alifanya ziara fupi mjini Tirana nchini Albania alikokutana na Waziri Mkuu wa Albania Sali Berisha.Kiongozi huyo alisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa kutimiza mipango ya kuipa uhuru Kosovo baada ya mazungumzo yao.

Wakazi wengi wa Kosovo wana asili ya Albania.Serbia na Urusi zinapinga mpango huo wa Umoja wa Mataifa huku Urusi ikitisha kukataza kisheria azimio lolote la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakaloruhusu jimbo la Kosovo kupata uhuru wake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com