1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sofia. Lula kuula tena awamu ya pili.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy5

Nchini Bulgaria rais aliyeko madarakani Georgi Paranov anaonekana kushinda awamu ya pili ya kipindi cha miaka mitano madarakani baada ya kuongoza katika uchaguzi wa duru ya pili unaofanyika leo.

Matokeo ya maoni yanampa kiongozi huyo msoshalist kati ya asilimia 75 na 80 ya kura dhidi ya asilimia 20 ya mpinzani wake Volen Siderov.

Wakati huo huo katika uchaguzi mwingine wa duru ya pili, rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anaonekana kupata ushindi wa kipindi kingine licha ya madai ya ulaji rushwa dhidi yake.

Utafiti wa maoni wa hivi karibuni unampa Lula kiasi cha asilimia 60 ya kura.