1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Snowden akataa masharti ya Urusi

2 Julai 2013

Mfanyakazi wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani Edward Snowden ameomba hifadhi ya kisiasa nchini Norway lakini uwezekano unaonekana mdogo kwa nchi hiyo kukubali.Snowden pia ameondoa ombi la hifadhi nchini Urusi.

https://p.dw.com/p/1906M
HONG KONG - 2013: (EDITOR'S NOTE: ONLY AVAILABLE TO NEWS ORGANISATIONS AND NOT FOR ENTERTAINMENT USE) In this handout photo provided by The Guardian, Edward Snowden speaks during an interview in Hong Kong. Snowden, a 29-year-old former technical assistant for the CIA, revealed details of top-secret surveillance conducted by the United States' National Security Agency regarding telecom data. (Photo by The Guardian via Getty Images)
Edward SnowdenPicha: The Guardian/Getty Images

Raia huyo wa Marekani Edward Snowden mwenye umri wa miaka 30, ambaye anakabiliwa na kesi ya kufanya ujasusi dhidi ya nchi yake, ameomba hifadhi ya kisiasa katika nchi 15 na anaendelea kuwapo katika eneo linalotumiwa na wasafiri kusubiri kuendelea na safari zao katika uwanja wa ndege wa mjini Moscow wa Sheremetyevo.

"Mtu kuomba hifadhi ya kisiasa akiwa hayupo katika nchi anayotaka kuishi , kimsingi haikubaliki," naibu waziri wa sheria wa Norway Paal Loenseth ameliambia shirika la habari la nchi hiyo NRK.

Russia's President Vladimir Putin smiles during a meeting in his residence in the Black Sea resort of Sochi, Russia, on February 5, 2013. Putin discussed today financial situation surrounding restoration works in Russia's southern town of Krymsk, severely affected by floods last summer. AFP PHOTO / POOL/ SERGEI KARPUKHIN (Photo credit should read SERGEI KARPUKHIN/AFP/Getty Images)
Rais Vladimir Putin wa UrusiPicha: S.Karpukhin/AFP/GettyImages

"Ombi la hifadhi ya kisiasa ni lazima lifanywe katika ardhi ya Norway. Kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida , ombi lake litakataliwa."

Hapo mapema wizara ya mambo ya kigeni imesema kuwa imepokea ombi kwa ajili ya hifadhi ya kisiasa kutoka kwa Snowden kwa njia ya fax katika ubalozi wake mjini Moscow mchana jana Jumatatu.

Wakati huo huo , "Snowden aliomba kuendelea kuishi nchini Urusi , lakini jana , baada ya kufahamu msimamo wa rais Putin kulingana na masharti ambayo anaweza kuishi nchini humo, aliondoa ombi lake," amesema msemaji wa rais Putin , Dmitry Peskov.

GettyImages 170293810 NEW YORK, NY - JUNE 10: A supporter holds a sign at a small rally in support of National Security Administration (NSA) whistleblower Edward Snowden in Manhattan's Union Square on June 10, 2013 in New York City. About 15 supporters attended the rally a day after Snowden's identity was revealed in the leak of the existence of NSA data mining operations. (Photo by Mario Tama/Getty Images)
Mtu mmoja akimuunga mkono SnowdenPicha: Getty Images

Snowden hataki masharti

"Kimantiki , Snowden anaweza kuishi katika shirikisho la Urusi kwa masharti kuwa anaachana na shughuli zake za kufichua taarifa za siri za Marekani. Kwa mujibu wa yale tunayoyafahamu , hataki kuachana na shughuli hizo, ameongeza msemaji huyo wa rais. Rais Putin amesema.

"Iwapo anataka kwenda kokote na atapokelewa huko anakotaka kwenda, tuko tayari kumruhusu. Iwapo anataka kubaki hapa nchini, tuna sharti moja; ni lazima aachane na shughuli zake zenye lengo la kuwadhuru washirika wetu, licha ya kuwa inaonekana si jambo la kawaida kwamba mimi ndio natamka maneno hayo."

Anakabiliwa na vikwazo kadha

Poland imekataa pia kumpokea Snowden , wakati maafisa nchini Ujerumani , Austria na Uswisi wamesema kuwa hawezi kupeleka maombi yake katika nchi hizo wakati yuko katika nchi nyingine.

A poster supporting Edward Snowden, a former contractor at the National Security Agency (NSA) who leaked revelations of U.S. electronic surveillance, is displayed at Hong Kong's financial central district June 17, 2013. Snowden reportedly flew to Hong Kong on May 20. He checked out of a luxury hotel on June 10 and his whereabouts remain unknown. Snowden has said he intends to stay in Hong Kong to fight any potential U.S. moves to extradite him. REUTERS/Bobby Yip (CHINA - Tags: POLITICS CRIME LAW SCIENCE TECHNOLOGY)
Bango linalounga mkono alichofanya Edward SnowdenPicha: Reuters

Tovuti inayofichua taarifa za siri ya Wikileaks imesema kuwa Snowden , ambaye anaamika kuwa yuko katika uwanja wa ndege mjini Moscow , ameomba hifadhi ya kisiasa katika nchi zipatazo 21 ikiwa ni pamoja na nchi 13 katika bara la Ulaya. Mataifa mengi ya Ulaya yanataka ombi kama hilo kufanywa katika ardhi ya nchi hizo na sio nje.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema leo kuwa Edward Snowden , anastahili "ulinzi wa dunia" kwa kutoa taarifa za mpango wa ujasusi wa Marekani.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / ape

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman