1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIRTE: Mkutano wa Darfur wasusiwa na JEM na SLA-Unity

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CK

Wajumbe wamekusanyika mji wa Sirte nchini Libya kuzindua majadiliano yanayolenga kumaliza mgogoro wa miaka minne na nusu katika jimbo la Sudan, Darfur.Lakini kuna shaka ikiwa mkutano huo utaweza kupata makubaliano ya maana,kwa sababu makundi makuu mawili ya waasi yamesusia mazungumzo hayo ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.