1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya maji duniani

Saumu Ramadhani Yusuf22 Machi 2010

Watu zaidi ya bilioni moja duniani wanakosa maji safi ya kunywa

https://p.dw.com/p/MZ1l
UN wa Mataifa umeeka lengo la kila mwanadamu kupata maji safi ya kunywa kufikia mwaka 2015.Je lengo hilo litafikiwa?Picha: picture-alliance/ dpa

Sehemu kubwa ya ardhi ya dunia imezungukwa na maji.Kwa hali hiyo inaweza kuonekana kwamba kuna kiasi cha kutosha cha maji katika dunia.Asilimia 97,5 ni maji ya bahari na mito pamoja na maziwa.Kiwango kilichosalia cha asilimia 2,5 ni maji maji safi.Takriban theluthi moja ya watu wote duniani hawana maji safi ya kunywa.Na idadi nyingine inagawanya kiasi cha maji kilichosalia.

Hii leo karibu watu billioni 1,1 duniani hawana maji safi ya kunywa na wengine wapatao billioni 2,6  ambao ni kiasi cha thuluthi moja ya watu wa dunia nzima  hawapati maji ya kutosha kukidhi huduma zao za siku kwa jumla.Katika malengo ya Millenium ya Umoja wa mataifa imezungumzwa kwamba, maji ni mojawapo ya bidhaa  muhimu inayotakiwa kuwafikia watu wote wa dunia kufikia mwaka 2015.

Data za shirika la maji nchini Ujerumani za mwaka 2008 zinaonyesha kwamba matumizi ya maji kwa siku yalifikia lita 122.Nchini Italia kiwango hicho ni lita 800 kwa kila mtu.Kwa mantiki hiyo imeonyesha kwamba matumizi  jumla ya maji yanazidi kuongezeka kila uchao.Maji yanatumika sio tu kwa matumizi ya kila siku ya majumbani bali hata kwenye mashamba kwa mfano ya mchele  kahawa au pamba.

BdT Indischer Farmer am Welt Wasser Tag
Ukame unatokana na ukosefu wa mvua na kusababisha pia ukosefu wa maji duniani.Picha: AP

Uchunguzi uliofanywa na shirika la linaloshughulikia mazingira la World wide Fund for Nature WWF unaonyesha kwamba kila mkaazi nchini Ujerumani anahitaji kiwango cha zaidi ya lita 5000 kwa matumizi yake jumla kwa siku.Ingawaje maji ni bidhaa muhimu katika maisha ya mwanadamu lakini bado imesalia kuwa bidhaa ghali kabisa  na ambayo haipatikani kiurahisi na kila mtu na pia ubora wake unatofautiana.Matatizo hayo ya maji sio tu yanashuhudiwa katika ulimwengu wa tatu bali ni tatizo la ulimwengu mzima kwa jumla.

Kuna maeneo  machache  duniani ambayo yana matatizo  sugu ya ukosefu wa maji nayo ni pamoja na eneo la Sahel mashariki ya kati na baadhi ya maeneo ya Asia.Nchi nyingi  zinazoendelea  hilo ni tatizo la kila siku.

Mwandishi Scheschkwewitz Daniel ZR/Saumu Mwasimba

Mhariri AbdulRahman,Mohammed