1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kupinga Mateso Duniani

26 Juni 2007

Hali ya mateso dhidi ya binaadamu inaendelea kushuhudiwa katika nchi nyingi duniani huku ulimwengu ukiadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa mkataba wa umoja wa mataifa wa kupinga mateso duniani.

https://p.dw.com/p/CHCD
Mtu aliyepata mateso nchini Zimbabwe
Mtu aliyepata mateso nchini ZimbabwePicha: Ludger Schadomsky

Mateso mengi dhidi ya binaadamu katika nchi za Afrika yanatokea zaidi katika nchi zilizo na mizozo hasa ya kisiasa kama vile Sudan,Somalia,Kongo na zinginezo.

Saumu Mwasimba amezungumza na mwanaharakai wa haki za binaadamu na vile vile mwanasheria nchini Tanzania Profesa Chris Peter ambaye kwanza anaeleza umuhimu wa siku hii ya kupinga mateso.