Siku ya kupambana na njaa ulimwenguni | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Siku ya kupambana na njaa ulimwenguni

Njaa inaweza kuepukwa anasema rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Horst Köhler

Rais wa shirikisho Horst Köhler na mkewe

Rais wa shirikisho Horst Köhler na mkewe

Umoja wa mataifa umeichagua Oktober 16, siku ya kuasisiwa shirika la Umoja wa mataifa la ardhi za kilimo na mifugo kua siku vya chakula ulimwenguni.

Miaka 11 baada ya mkutano wa kilele wa kimataifa mjini Roma, kuhusu chakula ulimwenguni,idadi ya wanaosuzmbuliwa kwa njaa ulimwenguni bado ni kubwa kupita kiasi-hayo ni ,kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa leo na shirika la chakula na kilimo la FAO.

Katika mataifa masikini ya dunia watu milioni 850 hawali chakula cha kutosha,katika nchi zinazoinukia wanaokumbwa bna ukosefu wa chakula ni watu milioni 25 na katika nchi tajiri kiviwanda watu milioni tisaa wanashinda na njaa au hawali chakula cha kutosha.”Katika dunia yetu ya utandawazi-masuala muhimu yanayohusu ubinaadam-amani,uhuru , chakula kwa wote-haki ya mtu kujiendeleza na kuhifadhiwa mazingira yetu-yanabidi yapatiwe ufumbuzi wa pamoja-“ amesema rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Horst Köhler katika hotuba yake mbele ya wawakilishi wa shirika la FAO mjini Roma.

Njaa si janga lisiloweza kuepukwa-anahoji rais wa shirikisho Horst Köhler,katika hotuba yake mbele ya umati wa watu waliojazana katika ukumbi wa shirika la kimataifa la chakula na kilimo FAO mjini Roma.

Njaa inaweza kuepukwa kama sera za hikma na busara zitafuatwa anasisitiza rais wa shirikisho Horst Köhler,akishadidia kila binaadam ana haki ya kupata chakula cha kutosha, kizuri kwa afya, na kinachoambatana na mila na utamaduni wake.

Katika mfumo wa kidemokrasi,serikali zinalazimika kuhakikisha mahitaji ya raia yanazingatiwa na kutekelezwa,anasema rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Horst Köhler aliyesifu ushirikiano kati ya mataifa ya Umoja wa Afrika katika ule utaratibu uliopewa jina “Ushirikiano mpya kwaajili ya maendeleo ya demokrasia barani Afrika na utawala bora kama ngao ya kupambana na njaa.

Rais Horst Köhler amezitaka nchi tajiri ziuangalie mwamko huu wa bara la Afrika kama fursa ya kubuni aina mpya ya ushirikiano.Kipa umbele cha ushirikiano iwe katika maeneo ya mashambani anasema rais Köhler.Katika maeneo hayo ambako idadi kubwa ya watu wasiokua na chakula cha kutosha wanaishi katika sehemu ya kusini ya dunia yetu,ndiko mahitaji ya kimsingi ya chakula yanakobidi yakatekelezwe.Rais Köhler anasema:

“Nani anaweza kweli kutegemea kwamba mkulima wa kawaida,atamudu kutumia akiba kununulia shamba na zana za kilimo ikiwa suala la urithi na haki ya kutumia ardhi halikupatiwa ufumbuzi.Vipi mkulima ataweza kununua mashini na mbegu akiwa hana njia ya kupata mikopo?Vipi wakulima wataweza kuuza bidhaa zao ikiwa hata njia hakuna na barabara hazipitiki mvua zinaponyesha?”

Waratibu na wasaidizi wao mara nyengine wamekua wakitanguliza mbele miradi mikubwa mikubwa.Na mashirika ya kimataifa ya misaada ya maendeleo hayakua yakitanguliza mbele sana mitindo ya kutoa misaada ili watu waweze kujisaidia.Wakaazi wa mashambani wanahitaji kupatiwa mafunzo ya kazi pia. Anasema rais Köhler.

Kwa maoni yake Ulaya imechangia pia katika kuzifanya shughuli za kilimo katika nchi maskini zilenge kilimo cha zao moja linalosafireishwa nchi za nje..Rais wa shirikisho anapendekeza mazao siku za mbele yawe yakiwanufaisha wakaazi wenyewe kwanza.Tija ya bidhaa za mashambani zinazouzwa ng’ambo,anasema rais Köhler,itabidi itunzwe kwa kutiwa njiani masharti bora ya ushuru wa forodha kwaajili ya maendeleo.

Nchi tajiri zinabidi zifungue milango ya masoko yao kwa bidhaa za kilimo kutoka nchi masikini za dunia na kupunguza kwa sehemu kubwa ushuru wa forodha.

 • Tarehe 16.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C7hY
 • Tarehe 16.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C7hY

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com