1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kimataifa ya jeshi la kulinda amani la UN

29 Mei 2014

Leo ni siku ya Kimataifa ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa,na siku hii inaadhimishwa katika nchi mbali mbali kwa kuutambua mchango wa jeshi hilo duniani kote.

https://p.dw.com/p/1C8q0
Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa
Jeshi la kulinda amani la Umoja wa MataifaPicha: AP

Maadhimisho ya siku hii yanafanyika chini ya kauli mbiu inayolitaja jeshi hilo kama kikosi cha amani,mabadiliko na kinachosimamia mustakabali mzuri.Aidha siku ya leo inaadhimishwa wakati ambapo sehemu mbali mbali za dunia zinashuhudia mapigano na migogoro ikiwemo barani Afrika.Kuangalia mafanikio ya juhudi hizo za kulinda amani za Umoja wa Mataifa Saumu Mwasimba amezungumza na mchambuzi wa masuala ya usalama katika taasisi ya Kimataifa ya mafunzo ya usalama ISS mjini Nairobi,Emanuel Kisiangani ambaye kwanza alikuwa na tathmini ifuatayo kuhusu juhudi hizo.
Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Josephat Charo