1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kimataifa dhidi ya ubaguzi

Oummilkheir21 Machi 2007

Ubeligiji harusi za watu elfu moja kuadhimisha siku ya kulaani ubaguzi

https://p.dw.com/p/CB58
Kitambulisho cha Ujerumani dhidi ya ubaguzi:"Wote tofauti -wote ni sawa
Kitambulisho cha Ujerumani dhidi ya ubaguzi:"Wote tofauti -wote ni sawa

Matusi,ubaguzi na matumizi ya nguvu dhidi ya wageni-ni sura ya kusikitisha inayojitokeza takriban katika nchi kadhaa,kama si zote za ulaya.Kwa bahati nzuri kuna watu pia wenye moyo waliosimama kidete dhidi ya ubaguzi.

Umoja wa Ulaya umepania kupambana na ubaguzi na chuki dhidi ya wageni.Na hata kama bado lengo hilo liko mbali kufikiwa,lakini kuna mwamko miongoni mwa jamii katika juhudi za kupambana na ubaguzi.Bibi mmoja mpita njia anasema:

“Muhimu zaidi ni watu kuheshimiana,mamoja huyu ana rangi gani ya mwili au ametokea wapi.”

Nchini Ubeligiji siku ya mapambano dhidi ya ubaguzi ulimwenguni inamsisimua kila anaesimuliwa,wenyeji sawa na wageni.Watu elfu moja,mabibi na mabwana wanapanga kuongozana leo usiku hadi ofisi ya diwani huko Saint Nicolas,katika mji mdogo wa jamii ya Flemmish kwenda kufunga ndowa ili kudhihirisha msimamo wao dhidi ya ubaguzi wa rangi.Uamuzi huo ni jibu kwa kisa cha ubaguzi kilichotokea mwishoni mwa mwaka jana ambapo wazungu sita walikataa kufingishwa ndowa na mtu mweusi.

Sherehe hizo kubwa za harusi zinazofanyika hii leo wakati walimwengu wanaadhimisha siku ya kulaani ubaguzi,zinafanyika hadharani na kuongozwa na msaidizi wa diwani,mwenye asili ya kiafrika Wouter Van Bellingen,ambae kisa kilichomfika kilizusha ghadhabu kote nchini Ubeligiji.

Wouter Van Bellingen,mwenye asili ya Rwanda ,amechaguliwa mwanachama wa baraza la mji kufuatia uchaguzi wa October mwaka jana,kwa tikiti ya chama kidogo kinachopigania utawala mkubwa wa ndani kwa jimbo la Flander.Pekee rangi ya mwili wake ndio inayomtenganisha na wa Flemish wengine milioni sita wa nchi hiyo.

Lakini walipoarifiwa tuu kwamba watafungishwa ndowa na mtu mweusi,,watu hao sita wa kutoka mtaa wa Saint Nicolas wakaamua wasioane tena.

“Ubaguzi si kitu kipya kwangu”-lakini hilo ni tatizo lao wenyewe-amesema mbunge huyo kijana.

Wouter Van Bellingen hata hivyo ameshangazwa zaidi na kishindo kilichosababishwa na kadhia hiyo.Barua elfu mbili ,na risala za SMS alizozipata tangu kisa hicho kilipojiri zinaendelea kugonga vichwa vya habari magazetini tangu mwezi uliopita.

Viongozi wa serikali za miji wameamua kuandaa sherehe na mihadhara hii leo kuhimiza hali ya kuvumiliana katika mji huo ambako chama acha siasa kali za mrengo wa kulia Vlams Belang kilijikingia asili mia 26 uchaguzi ulipoitishwa October mwaka jana.

Katika daraja ya Umoja wa Ulaya,waziri wa sheria wa Ujerumani bibi Brigitte Zyprisse anasema:

“Tunataka kuhakikisha yeyote anaechochea hisia za chuki na matumizi ya nguvu chini ya misingi ya kikabila,anaadhibiwa.”

Mjini Saint Nicolas ,karibu na Antwerpes mamia ya watu watakaohudhuria sherehe za kufungishwa ndowa watu elfu moja na Wouter Van Bellingen,watafungua sherehe zao kwa mabusu kabla ya kukaribishwa katika karamu ambapo mapishi ya kutoka kila pembe ya dunia yataandaliwa.