1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku 100 za madaraka ya katibu mkuu mpya wa umoja wa mataifa.

Sekione Kitojo9 Aprili 2007

Mwishoni mwa mwaka jana Ban Ki Moon alirithi kiti alichokuwa akikalia Kofi Annan kama katibu mkuu wa umoja wa mataifa. Mwanadiplomasia huyu kutoka Korea ya kusini katika wadhifa wake wa sasa baadhi ya malengo yaliyoko mbele yake ni kutotaka kungoja ngoja. Hali ambayo Ban hadi sasa bado hajaweza kuitekeleza. Martina Buttler anaelezea baada ya kuwa karibu na kiongozi huyo kwa muda.

https://p.dw.com/p/CHGg

Siku mia moja, na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon bado ni mgeni katika medani ya kimataifa. Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert alimsalimia wakati wa ziara ya mashariki ya kati mwishoni mwa mwezi wa March kama katibu mkuu Moon, kiongozi mwenzake wa Lebanon alimtaja kama Bwana Annan. Ban Ki Moon kwa kweli hana kitu ambacho anaweza kutambulika nacho, licha ya kuwa ametoa ahadi kadha.

Katika muda wa miezi mitatu ijayo nitakuwa na kazi shughuli nyingi.

Pamoja na hayo katika siku ya kwanza katika makao yake makuu katika eneo la East River amesisitiza kuwa ni uzito gani maneno yake hadi sasa yamekuwa. Kama ilivyokuwa baada ya hukumu ya kunyongwa ya Saddam Hussein , alivyosisitiza kuwa kila nchi inapaswa kujiamulia mambo yake, iwapo iendeleze hukumu ya kifo, aliweza kupambana na tukio la kwanza la wimbi la ukosoaji. Hatimaye msimamo wa umoja wa mataifa kuhusu kupinga hukumu ya kifo hadi sasa imethibitishwa zaidi. Ban ni lazima arudi nyuma.

Pia siasa zake na uchaguzi wake katika nafasi za juu unashangaza.

Kuna hali inayofanana sana na Kofi Annan mwishoni mwa muda wake wa utawala wa miaka kumi na wiki kumi za mwanzo za utawala wa Ban Ki Moon. Lakini pia mwanzo wa Annan ulikuwa kwa kiasi fulani ukiyumba yumba. Mtu anapaswa kwa kweli kupata kazi ya kufanya haraka.

Hii pia si kitu cha kawaida, anasema Edward Luck, mtaalamu wa masuala ya umoja wa mataifa kutoka katika chuo kikuu cha Colombia.

Ban ana maswala makuu, ambayo yako katika agenda za dunia ambayo anayajua. Ziara yake ya kwanza alikwenda kukutana na viongozi wa umoja wa Afrika. Mjini Berlin , aliongoza mkutano wa wawakilishi wa kundi linalofanya majadiliano kuhusu mashariki ya kati. Walijadili, juu ya jinsi ya kupata amani baina ya Waplestina na Waisrael. Katika ziara yake ya mashariki ya kati lilianguka kombora mita chache karibu na alipokuwa wakati akiwa mjini Baghdad. Ban anatafuta pamoja na mambo mengine kujiweka binafsi katika hali nzuri, kama hali ya mambo inavyojionyesha nchini Iraq.

Anajaribu kujifunza haraka matatizo ya kulimwengu. Anaangalia katika maeneo kadha , ili kujua ni kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.

Anawakumbusha watu anaozungumza nao , kuwa tayari ameweka mambo yake muhimu na kama inavyoonyesha , huenda akaweza kushughulikia mzozo mwingine.

Mzozo wa jimbo la Darfur nchini Sudan kutokea siku yake ya kwanza ulikuwa katika orodha ya mambo muhimu. Na Ban kama kazi yake inayojionyesha, anafanya upatanisho baina ya makundi , anazungumza na kungalia faili za kidiplomasia. Na hili mara moja aliwahi kupiga ngumi mezani, kitu ambacho hakikutarajiwa kutoka kwake, kama anavyojitaja kuwa kuwa ni mtu wa kuweka mambo sawa. Mara nyingi anatoa nafasi lakini pia hutoa maelezo sahihi.

Tunabaki tukingoja, iwapo na lini litatoka kutoka kwake neno halisi. Kwa hakika yeye ni chombo pekee, ambako kama katibu mkuu wa umoja wa mataifa ana wajibu wa kuongoza maadili mema duniani.