1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria mpya kuleta upatanisho Irak

4 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1rY

BAGHDAD:

Sheria mpya ya Upatanisho na Haki itaanza kutumika nchini Irak baada ya kuidhinishwa na Baraza la Urais siku ya Jumapili.Sheria hiyo mpya ikitazamia kuleta upatanisho wa taifa,inawapa kiasi ya watu 40,000 waliokuwa wanachama wa zamani wa Baath Party cha Saddam Hussein uwezo wa kurejea katika kazi zao za zamani serikalini.Watu hao walifukuzwa kazi baada ya uvamizi wa Marekani nchini Irak na Saddam kuondoshwa madarakani.Wale waliostaafu wataweza kudai pensheni zao kwa serikali.