SHANGHAI:Kimbunga Wipha chagonga eneo la pwani | Habari za Ulimwengu | DW | 19.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SHANGHAI:Kimbunga Wipha chagonga eneo la pwani

Kimbunga Wipha kimepiga eneo la pwani lililo kusini mwa mji wa Shangahi mapema hii leo huku serikali ikiendelea na shughuli ya kuwaondoa wakazi milioni 2 wa maeneo ya pwani.Kulingana na utabiri wa hali ya hewa kimbunga hicho ndiyo kibaya zaidi kuwahi kupiga eneo la mashariki mwa Uchina katika kipindi cha muongo mmoja.Shule zimefungwa na huduma zote za usafiri kusitishwa katika mji mkubwa wa Uchina kufuatia onyo la mvua kubwa kutokea zilizoambatana na pepo kali.Dhoruba hiyo iligonga eneo la Cangnan kusini mwa mkoa wa Zhejiang na kuripotiwa kupungua nguvu kilipofika maeneo ya pwani kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa.Barabara za miji kadhaa zinaripotiwa kujaa maji.

Uongozi katika mikoa ya Shanghai,Zhejiang na Fujian umeagiza wakazi milioni 2 kwenye meli na maeneo ya pwani kuondoka.Kimbunga hicho kinaripotiwa kuwa na pepo zilizo na kasi ya kilomita 230 kwa saa ila kupungua nguvu kilipofika maeneo ya kaskazini ya pwani.Hakuna taarifa zozote za majeruhi au uharibifu mkubwa uliosababishwa na kimbunga hicho katika eneo la bara la Uchina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com