1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio mjini Baghdad

Oumilkher Hamidou4 Januari 2009

Damu yamwagika katika wakati ambapo washiya wajiandaa kwa siku kuu ya Ashura

https://p.dw.com/p/GRoz

Baghdad:

 Watu 40 wameuwawa baada ya bibi mmoja kujiripua  karibu na kiunga cha makaburi ya washiya,kaskazini magharibi ya mji mkuu wa Iraq  Baghdad.Watu wasiopungua 50 wamejeruhiwa.Shambulio hilo limetokea katika kituo cha karibu na Quba la imam Musa,katika mtaa wa Kadhimiya,wanakoishi waumini wengi wa madhehebu ya shiya.Waumini wengi walikua wakijiandaa katika sehemu hiyo kwaajili ya kuadhimisha siku kuu ya Ashura itakayoanza wiki hii.