1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali yafanya mazungumzo na wasaidizi wa al-Sadr.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVZt

Basra.

Serikali ya Iraq inafanya mazungumzo na wasaidizi wa kiongozi wa kidini Moqtada al-Sadr katika juhudi za kumaliza mzozo mjini Basra ambako majeshi ya serikali ya Iraq wanapambana na wanamgambo wa Kishia.

Msaidizi wa al-Sadr amesema leo Alhamis kuwa mazungumzo hayo yanafanyika katika mji wa Najaf.

Waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki amekuwa akiongoza operesheni hiyo dhidi ya wanamgambo wa jeshi la Mehdi mjini Basra tangu siku ya Jumanne.

Mapigano hayo yamesambaa katika maeneo mengine ya Washia, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Baghdad, huku watu zaidi ya 50 wameuwawa katika muda wa siku tatu.

Jana Jumatano al-Sadr amedai kuwa al-Maliki aondoke kwanza mjini Basra na kutuma ujumbe wa bunge kwa mazungumzo ya kutanzua mzozo huo.