1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Sri Lanka yatuhumiwa kuwateka nyara vijana wa Kitamil

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJiV

NEW YORK:

Majeshi ya ya usalama ya Sri Lanka na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wametuhumiwa kuwateka nyara mamia ya watu tangu mwaka 2006.Ripoti ya Shirika linalotetea haki za binadamu duniani,Human Rights Watch imesema,serikali ya Sri Lanka imehusika na kutoweka kwa watu na wengi wao ni wanaume vijana wa Kitamil wanaoshukiwa kuhusika na waasi wa Tamil Tigers.

Serikali ya Sri Lanka imesema,ripoti hiyo imetia chumvi ukweli wa mambo.Maelfu ya watu wameuawa kisiwani Sri Lanka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea tangu zaidi ya miaka thelathini kati ya majeshi ya serikali na waasi wa Tamil Tigers.