1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Rwanda yatoa maoni yake kuhusu Kukamatwa kwa waasi wa FDLR nchini Ujerumani

18 Novemba 2009

Nchini Rwanda,Serikali imekaribisha hatua ya Ujerumani kuwakamata viongozi wawili wa kundi la waasi wa kihutu la FDLR wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/KaFC

Kiongozi wa kundi hilo, Ignace Murwanashaka mwenye umri wa miaka 46 alikamatwa katika mji wa Karlsruhe, huku naibu wake Straton Musoni mwenye umri wa miaka 48 akikamatwa katika mji wa Stuttgart hapa Ujerumani. Serikali ya Rwanda imesema kukamatwa kwa wawili hao ni hatua nzuri katika kuhakikisha haki inatekelezwa kwa waathiriwa wa maovu hayo nchini Rwanda na Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Kutoka mji wa Kigali mwandishi wetu Daniel Gakuba anafuatilia tukio hilo na hii hapa ripoti yake kamili.

Mtayarishaji:Daniel Gakuba

Mpitiaji:Jane Nyingi