1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Mpito katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

Oumilkheir Hamidou
18 Novemba 2016

Hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,kishindo katika korti ya mjini The Hague baada ya nchi kadhaa za Afrika kuamua kubatilisha mkataba wa Rome na mizozo ya kiuchumi na rushwa zazidisha kero za waafrika Magazetini

https://p.dw.com/p/2St6z
Demokratische Republik Kongo Joseph Kabila
Picha: Getty Images/AFP/J.D. Kannah

 

Tunaanza lakini na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ambako wiki hii mwanasiasa wa upande wa upinzani Samy Badibanga aliteuliwa kuwa waziri mkuu kuambatana na makubaliano ya kisiasa. Kabla ya hapo  lilikuwa die Tageszeitung lililoandika kuhusu kuzidi makali mvutano mjini Kinshasa. Lilizungumzia kuhusu serikali kujiuzulu na mpango wa kuundwa serikali ya mpito. Lakini rais Joseph Kabila limeendelea kuandika gazeti hilo hajafichua chochote kuhusu dhamiri zake,muda mfupi kabla ya mhula wake kumalizika. Serikali ya mpito itaiongoza jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kuelekea chaguzi za rais na bunge zitakazoitishwa April mwaka 2018.

 Hadi uchaguzi mpya utakapoitishwa,rais Kabila anapanga kuendelea kuwepo madarakani ingawa,kwa mujibu wa katiba mhula wake unamalizika decemba 19 inayokuja. Kuna uwezekano kwa hivyo Kabila akataka kugombea tena kiti cha urais, uchaguzi mpya utakapoitishwa,kinyume na katiba,limemaliza kuandika die Tageszeitung.

Korti ya kimataifa ya uhalifu yaagubikwa na kishindo

"Korti ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague yagubikwa na kishindo" ndio kichwa cha maneno cha gazeti la Neues Deutschland lililozungumzia mashauriano yaliyotishwa kuzungumzia mustakbal wa korti hiyo. Baada ya mataifa kadhaa ya Afrika kutangaza kujitoa katika korti hiyo ya kimataifa wawakilishi kutoka mataifa 124 wanachama walikutana jumatano iliyopita kwa mkutano wao wa mwaka mjini The Hague. Gazeti la Neues Deutschland linasema ilikuwa mbinu pale mwendesha mashitaka mkuu Fatou Ben Souda alipoitaja ripoti ya wachunguzi wa kimataifa nchini Afghanistan, muda mfupi kabla ya mkutano huo wa mwaka,inayozungumzia kuhusu uhalifu wa vita uliofanywa na wanajeshi wa Marekani na watumishi wa shirika la upelelezi la Marekani CIA.

Gazeti la Neues Deutschland linajiuliza kama hiyo si mbinu ya mwendesha mashitaka mkuu Fatou Ben Souda kwakua Marekani,sawa na Urusi, China na Israel hawakuidhinishja makubaliano ya Rome yaliyopelekea kuundwa korti hiyo ya kimataifa ya mjini The Hague na hadi wakati huu ni wanasiasa na mabwana vita wa Afrika tu ndio wa Afrika ndio walioketi katika kiti moto cha mahakamana hiyo-watano wameshahukumiwa hali iliyozusha malalamiko barani Afrika na kupelekea mataifa mfano wa Afrika Kusini, Burundi, Gambia alikotokea Fatou Bensouda kutangaza kubatilisha mkataba wa Roma. Uamuzi wa kujitoa mataifa ya Afrika katika korti ya kimataifa ya uhalifu ni pigo kwa wahanga wa matumizi ya nguvu barani Afrika,limeandika Neues Deutschland lililomnukuu mtaalam wa sheria za kimataifa kutoka Tanzania Benjamin Aluka.

Rushwa na ukosefu wa ajira ni miongoni mwa kero za waafrika

Mzozo wa kiuchumi barani Afrika pia ulimulikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani wiki hii. Katika ripoti yake Frankfurter Allgemeine linasema mzozo wa kiuchumi na rushwa ndio mambo yanayowakera zaidi waafrika. Katika madola makuu ya kiuchumi kusini mwa jangwa la Sahara kero zimezidi tangu mwaka mmoja uliopita. Asili mia 70 ya wakaazi wa Afrika Kusini na Nigeria wanalalamika wakisema hali ya kiuchumi katika nchi zao ni mbaya. Na hasa nafasi duni za kazi ndio inayoangaliwa kuwa chanzo kikubwa cha hali hiyo. Malalamiko makubwa pia yanatolewa kuhusu rushwa. Serikali zinawatajirisha baadhi tu ya makundi ya kijamii ni miongoni mwa lawama zinazosikika-Hayo yanatokana na uchunguzi wa maoni ya umma uliosimamiwa na kituo cha utafiti cha Marekani-Pew Research Center.

Nigeria ambayo kutokana na wakaazi wake milioni 185 ndio nchi yenye wakaazi wengi zaidi barani Afrika,asili mia 93 walioulizwa maoni yao wanaitaja hali ya umaskini, uhaba wa nishati, uhalifu, maafisa mafisadi wa serikali na ukosefu wa ajira ndio sababu za kero zao kubwa. Nchini Kenya,nchi ya tatu,baada ya Afrika kusini ambako shirika hilo la Marekani liliongoza uchunguzi wake asili mia 91 wanalalamika wakisema rushwa ndio tatizo kubwa, ikifuatiwa na ukosefu wa ajira, umaskini na uhalifu.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/BASIS/PRESSER/ALL

Mhariri: Grace Patricia Kabogo