1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Burundi kususia mazungumzo ya amani

Sekione Kitojo
16 Februari 2017

Serikali ya Burundi imesema haitahudhuria mazungumzo ya  amani yaliyopangwa kuanza tena nchini Tanzania, licha ya muungano mkuu wa upinzani kuthibitisha kwamba utashiriki.

https://p.dw.com/p/2XgOk
Burundi Präsident Pierre Nkurunziza
Picha: Getty Images/AFP/F.Guillot

 Mazungumzo hayo yanalenga kutafuta suluhu katika mzozo wa kisiasa uliosababisha umwagikaji wa damu ambao ulianza mwaka 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunziza kusema atawania muhula wa tatu madarakani, hatua ambayo wapinzani wamesema inakiuka  katiba na makubaliano ya amani yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Serikali imekuwa  ikiushutumu Umoja wa Mataifa kwa kufanya upendeleo dhidi yake baada ya makundi kadhaa ya haki za binadamu kusema majeshi ya usalama na chama tawala yamejihusisha na ukiukaji mkubwa wa haki za  binadamu. Msemaji wa serikali Phillipe Nzobonariba amesema serikali inapinga kuwapo kwa mshauri  mwandamizi wa Umoja wa  Mataifa Benomar Jamal katika mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Arusha,Tanzania.