1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali kuu ya Muungano siku 100 Madarakani Berlin

26 Machi 2014

Siku 100 za serikali ya muungano wa vyama vikuu mjini Berlin,sheria mpya ya halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya kuhusu mazao ya "Bio" na Bayern Munich kutawazwa mabingwa wa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani magazetini

https://p.dw.com/p/1BVrZ
Kikao cha baraza la mawaziri walipokuwa wanakula kiapo disemba 17 mwaka 2013Picha: picture-alliance/dpa

Tunaanzia Berlin kumulika siku mia moja tangu serikali ya muungano wa vyama vya kihafidhina vya Christian Democratic Union-CDU,Chrisian Social Union CSU na wasocial Democrats wa SPD ilipoingia madarakani.Hawakuanza vibaya,hakuna malumbano hata kashfa ya Edathy haikuwatia kishindo au washirika wadogo SPD ndio wanaong'ara" ni miongoni mwa vichwa vya habari habari magazetini .Gazeti la "Münchner Mercur" linaandika:"Siku mia moja za muungano wa vyama vikuu zinabainisha wasoshial Democrat ndio walioshinda mashindano ya awamu hii ya kwanza madarakani.Hakuna aliyewapita:naiwe katika suala la malipo ya uzeeni,kiwango cha chini cha mshahara,malipo ziada kwa wazee au kuwekewa kikomo kodi za nyumba....Sote tunabidi tutambue kwamba tija ya uchaguzi wa leo,watoto na wajukuu zetu ndio watakaotakiwa wailipie kesho.Hapo serikali ina nafasi ya kurekebisha mambo sawa na vile inavyopaswa irekebishe katika suala la mageuzi ya nishati.

Mtaka cha Mvunguni huinama

Imani ya mnunuzi imepungua linapohusika suala la mazao ya "Bio" au yale mazao ambayo tangu mwanzo mpaka mwisho hayatumiliwi mbolea za sumu na kadhalika.Ili kutuliza hofu za wanunuzi na kurejesha imani,halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya imetangaza sheria mpya.Gazeti la "Esslinger Zeitung" linaandika: " Ni sawa kabisa kuiona halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya inawajibika na kutangaza viwango vya chini kabisa vya mabaki ya dawa ya kuuwa wadudu waharibifu katika mazao ya Bio.Kwamba baadae mazao hayo yanabidi yachunguzwe,si suala la kuulizwa! Usalama wa wanunuzi hauwezekani bila ya urasimu.Mtaka cha mvunguni huinama.Kila mmoja atabidi atambue ,akitaka "Bio" atabidi alipie " Bio".

Biosiegel auf einer Packung Kresse
Mbonga na mhuri wa BioPicha: picture-alliance/dpa

Bayern Munich watawazwa kwa mara ya 24 mabingwa wa ligi kuu

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu kabumbu.Jana usiku timu mashuhuri ya Ujerumani Bayern Munich imevikwa taji la ubingwa wa ligi kuu -Bundesliga hata kabla ya michuano kumalizika.Gazeti la "Berliner Morgenpost" linaandika:" Kama ilivyokuwa ikitarajiwa,watoto wa FC Bayern Munich wamenyakuwa taji la mabingwa wa ligi kuu.Kwa wengi wa mashabiki wake lakini taji hilo la 24 katika historia ya Bayern Munich lilitiwa ila kidogo.Hata hivyo ni jambo la kawaida kwa kila kitu kutiwa ila humu nchini.Kuna wanaowamezea mate na wengine wanaowaonea kijicho.

Fußball Bundesliga - Der FC Bayern München ist Meister
Watoto wa Bayern Munich wanyanyuwa taji la ubingwa wa ligi kuuPicha: Getty Images

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman