1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serengeti- Safari kuelekea kusikojulikana

17 Aprili 2014

Tunakupeleka pamoja nasi katika ulimwengu wa kuvutia: Jionee simba wanaounguruma, pundamilia wanaobweka na maelfu ya nyumbu - katika safari yetu ndani ya Serengeti.

https://p.dw.com/p/1Bjzj

Leo warithi wao wanaisimamia mbuga hiyo ya taifa. Timu ya Afrika ya Jumuiya ya Kutunza Wanyama ya Frankfurt (FZS) inatoa kipaumbele cha juu kabisa kwa mbuga ya wanyama ya Serenegeti. Na leo hii, Serengeti ni miongoni mwa mbuga za wanyama zenye ulinzi bora zaidi duniani. Lakini maisha ya wanyamapori huko yanazihisi athari za ulimwengu wa kisasa. Hiyo inatoa changamoto kwa watunzaji wa wanyama. Kwa mfano, jumuiya ya FZS iliweza kuzuwia ujenzi wa barabara kuu kupitia katika mbuga hiyo. Barabara hiyo ingeweza kuvuruga uhamaji wa wanyama na kuharibu mfumo wa ikolojia wa Seregenti katika muundo wake wa sasa.

Mbuga hii hufadhiliwa kwa kiasi kikubwa kupitia malipo yanayotozwa kwa wageni. Kiasi kingine cha euro milioni moja kutoka mjini Frankfurt kila mwaka, hutumiwa katika ulinzi wa Serengeti. FZS inatumia fedha hizo kuisaidia Mamlaka ya Mbuga za Wanyamapori ya Tanzania (TANAPA) katika programu zake za mafunzo na uendeshaji, au kuipatia vifa vya ufundi kama vile magari yanayotumiwa na wasimamizi wa mbuga. Bila ushirikiano huu na kujitolea bila kuchoka kwa wahifadhi, wanyama wa Serengeti wangekabiliwa tena na maangamizi.

Njoo ujiunge nasi katika safari ndani ya pepo hii ya wanyama ya Tanzania yenye kuvutia lakini inayokabiliwa na kitisho: Jionee simba wanaounguruma, pundamilia wanaobweka na maelfu ya nyumbu - katika safari yetu ndani ya Serengeti.