1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sera ya mazingira ya Ujerumani

17 Januari 2008

Ujerumani kinyume na nchi nyengine za kiviwanda ina mradi wa kuachana kabisa na vinu vya nishati ya nuklia.

https://p.dw.com/p/Ct1J

Viwanda vya nishati ya kinuklia vya Ulaya vinacheka na kufurahi wakati huu:Kwanini ? Uingereza,ina azma ya kujenga vinu vipya vya kinuklia. Ufaransa na Finland tayari kizazi kipya cha mitambo ya vinu vya nishati ya kinuklia inaundwa.China nayo imapanga mnamo miaka 15 ijayo kujenga vinu 30 vya nishati ya nuklia.

Kiwanda cha vinu vya kinuklia cha Ufaransa (AREVA) kinazungumzia upepo mpya unaovuma katika soko la nishati.Kinyume na nchi hizo nyengine, kuachana kabisa na nishati ya nuklia ni jambo lililokwishaamuliwa na yadhihirika hakuna kurudi nyuma.Mabingwa wa hali ya hewa na mazingira wanaonya juu ya gharama na hatari kubwa zitakazotokana na kujitanua huko kwa vinu vya nuklia.

Swali lakini,kutokana na mipango hiyo ya kustawisha vinu vya nishati ya nuklia,itawezekana kuzifitimiza shabaha za ulinzi na usafi wa mazingira zilizowekwa ?

Katika mkutano wa mazingira hapo desemba mwaka jana huko bali, Indonesia,waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel aliweza kunawiri kwa mchango wake aliotoa.Hakuna nchi nyengine kama asemavyo Bw.Gabriel inayotekeleza juhudi za kutunza mazingira zilizoafikiwa kama Ujerumani.Hadi ifikapo 2020 Ujerumani itapunguza hadi 40% ya moshi wake unaopaa hewani kutoka viwanda vyake.Itafanya hivyo kupitia nishati nyengine inayoweza kutumika tena-renewable energy, kupitia kupunguza matumizi na kwa njia pia ya kutia raslimali ya mabilioni ya Euro katika kukarabati majumba,matumizi safi ya makaa ya mawe na vinu vinavyotumia gesi.Umeme kutoka nishati ya vinu vya atomiki itabakia kuwa mwiko.Alao hiyo ndio shabaha ya muda unaokuja.

Hadi itapofika 2021 vinu vyote 17 vya nishati ya nuklia vitafungwa hatua kwa hatua.

Kwa kuchukua msimamo huo,Ujerumani inajikuta inasimama pekee miongoni mwa dola za viwanda .Nchini Finnland vinu vipya vya nishati ya nuklia vinajengwa.Nchini Ufaransa halkadhalika sawa na ilivyo Marekani na japan.Uingereza hivi punde imeaamua kutoka sasa kutegemea zaidi nishati ya kinuklia.Serikali za nchi hizi zinatoa hoja kwamba ni kwa kutumia vinu vya nishati isiopaza moshi unaochafua mazingira hewani, ndipo itayumkinika kuzifikia shabaha zilizowekwa na Jumuiya ya kimataifa-shbaha ambazo hata wataalamu wa sayansi ya hali ya hewa wanadai hazitoshi kuzima hatari za uchafuzi wa mazingira.

Hatahivyo,ikiwa ujerumani itazidi kuachana na nishati ya nuklia,hii ina sababu zake njema:

Kiasi cha vinu vya nuklia 440 katika nchi 31 zinazalisha wakati huu kiasi cha 16% ya mahitaji ya umeme ulimwenguni.Uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na moshi kupambana nao, inabidi kuwa na vinu vya nishati ya kinuklia 1000.Hii haionekani kufanyika karibuni.

Muhimu zaidi raslimali za kujenga vinu vipya vya nishati ya nuklia itagharimu fedha nyingi na madini ya mali-ghyafi inayotakikana -uranium ni rahisi.Vinu vya nishati ya nuklia vinahitaji muda mrefu kwa waekezaji kuweza kujipatia faida.

Lakini ikiwa wasemayo wataalamu wa hali ya hewa ni sawa, hadi ifikapo 2020 lazima moshi unaochafua mazingira lazima uwe umepungua ili kunusuru hali ya hewa ulimwenguni kuchafuka zaidi.

Na katika upande huu ndipo nchi nyingi zinaelekea kutumia nishati ya nuklia.

Ujerumani kwa kila hali, imeamua bila kigeugeu kunyosha njia yake na kuachana na nishati ya nuklia na kutumia teknolojia ya kutunza mazingira bila nishati ya nuklia.iaka ijayo itaamua pale Ujerumani itakapotoa ushahidi kuwa njia zote mbili zawezekana kujitolea kulinda mazingira na kuachana na nishati ya nuklia,basi nchi nyengine zitapaswa kufuata mfano wa Ujerumani.La sihivyo, vinu zaidi vya nishati ya nuklia vitaibuka alao katika nchi za kiviwanda,nchini India,China au hata Brazil.Kwani, kwa nchi masikini kama zile za bara la Afrika, nishati ya vinu vya nuklia hazimudu.