1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SEOUL: Waziri mkuu wa Japan ziarani Korea Kusini

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amewasili mjini Seoul kukutana na rais wa Korea ya Kusini, Roh Moo-hyun.

Mazungumzo yao yatatuwama juu ya kuboresha uhusiano kati ya serikali zao na pia kuishawishi Korea ya Kaskazini isiendelee na mpango wake wa kutengeza silaha za kinyuklia.

Hapo awali waziri mkuu Shinzo Abe alizuru China ambako alikutana na rais wa nchi hiyo Hu Jintao mjini Beijing. Rais Hu Jintao alisema ana matumaini kwamba ziara ya waziri mkuu Abe itaboresha uhusiano na kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo.

Viongozi wote wawili wamekubaliana kuwa jaribio la nyuklia la Korea ya Kaskazini haliwezi kuvumilika na serikali ya Pyongyang inatakiwa irudi kwenye mazungumzo juu ya mpango wake wa nyuklia bila masharti.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com