Seoul. Viongozi wa Korea wakutana. | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Seoul. Viongozi wa Korea wakutana.

Marais wa Korea ya kusini na kaskazini wamekutana kwa na mazungumzo rasmi katika muda wa miaka saba. Rais wa Korea ya kusini Roh Moo-hyun na mwenzake wa Korea ya kaskazini Kim Jong Il wamekutana katika nyumba ya wageni ya Paekhwawon ambako rais Roh amefikia. Agenda rasmi imetolewa kwa mkutano huo wa pili katika historia ya nchi hiyo ya kikomunist ya kaskazini na ile ya kibepari ya upande wa kusini. Lakini serikali ya Korea ya kusini imesema kuwa hali bora na amani ni mada ambazo zitakuwa muhimu katika mkutano huo wa siku tatu baina ya mataifa hayo mawili ambayo kiufundi yako vitani kufuatia mzozo wao wa mwaka 1950 hadi 53. Rais wa Korea ya kusini Roh Moo-hyun amesema kuwa anataka mkutano huo kupunguza hali ya wasi wasi na kusaidia uchumi wa nchi hiyo jirani ya kikomunist.

Roh , akiwa na miezi mitano tu ya kubaki madarakani , amesema kuwa kipaumbe anakitoa kwa kuleta amani katika eneo hilo na huenda akatoa ombi la kutia saini aina fulani ya taarifa za amani na Korea ya kaskazini. Wakati huo huo Marekani imesema kuwa imeidhinisha makubaliano ya majaribio yaliyofikiwa katika mkutano wa nchi sita, uliokuwa chini ya uenyeji wa China, ambapo yatasitisha shughuli za vinu vya kinuklia katika eneo la Yongbyon nchini Korea ya kaskazini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com