1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL. Korea Kusini yaihimiza jirani yake irudi katika mazunmgumzo ya pande sita

12 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3U

Bunge la Korea Kusini leo limepitisha azimio la kulaani jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini. Korea Kusini imeitaka Korea kaskazini kurudi katika mazungumzo ya pande sita yaliyokwama ili kujadili mpango wake wa nyuklia. Makamu kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Yong-Nam amesema kuwa vikwazo dhidi ya nchi yake vitazuia kuregelea mazungumzo hayo ya pande sita.

Wakati huo huo wawakilishi wa Japan na China wamesema kuwa hadi sasa hakuna athari zozote zilizojitokeza baada ya jaribio la kinyuklia la Korea Kaskazini, lakini hata hivyo Japan imeunga mkono azimio la kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini vikiwemo vya silaha na usafiri pamoja na Japan kusimamisha uagizaji wa bidhaa kutoka nchi hiyo Japan pia imezipiga marufuku meli zote za Korea Kaskazini katika bahari ya Japan. Katika mswada huo mpya wa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini Marekani lakini imelegeza lugha yake katika maswala ya ukaguzi wa shehena na fedha, hiyo ni kwa sababu ya kuzishawishi Urusi na China ziunge mkono mswada huo wa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Liu Yian Chao amesema.. O ton….Lengo letu sio kuiadhibu Korea Kaskazini bali yale tunayoyafanya ni kutafuta suluhisho na kujaribu kuirudisha nchi hiyo katika mazungumzo ya pande sita. Katika dunia hii ni bora kila tatizo litatuliwe kwa njia ya amani na mazungumzo.