1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEMARANG: Watu zaidi ya 500 hawajulikani waliko

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCed

Watu zaidi ya 500 hawajulikani waliko baada ya feri kuzama katika pwani ya kisiwa cha Java nchini Indonesia. Feri hiyo ilizama kufuatia tufani hapo jana ilipokuwa njiani kwenda bandari ya Semarang kisiwani Java ikitokea kisiwa cha Borneo.

Waziri wa uchukuzi nchini Indonesia amesema zaidi ya manusura 10 wameokolewa kutoka bahari hiyo iliyochafuka. Inaaminiwa feri hiyo ilikuwa imewabeba abiria zaidi ya 600.