SDE BOKER : Olmert tayari kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina | Habari za Ulimwengu | DW | 27.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SDE BOKER : Olmert tayari kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema leo Israel itakuwa tayari kuwaachilia wafungwa wengi wa Kipalestina wakiwemo wale wanaotumikia vifungo vya muda mrefu ili badala yake wanamgambo wamwachilie huru mwanajeshi wa Israel waliemteka hapo mwezi wa Juni.

Katika hotuba kuu ya sera Olmert amesema amekuwa akiwasihi Wapalestina juu ya amani na kupendekeza kutowa vifuta jasho kadhaa vya kibinaadamu na kiuchumi ikiwa matumizi ya nguvu dhidi ya Israel yatakomeshwa.

Hata hivyo ameweka masharti ya kuanzishwa upya kwa mazungumzo yoyote yale ya amani kwa kuachiliwa kwa askari huyo na kukubali kwa serikali yoyote ile ya umoja wa kitaifa ya Palestina ya kipindi cha usoni madai ya kimataifa ya kukanusha matumizi ya nguvu,kuitambuwa Israel na kukubali makubaliano ya amani yalioko hivi sasa kati ya Israel na Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com