Schalke 04 | Michezo | DW | 13.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Schalke 04

Schalke 04 ilitawazwa mara ya mwisho mabingwa wa Ujerumani, 1958 kabla kuanzishwa kwa Bundesliga,1963.Tangu enzi hizo,Schalke inajitahidi kuvaa tena taji lakini inaanguka hatua ya mwisho.

Schalke 04- ni timu iliopigiwa sana upatu mara nyingi miaka ya karibuni kuipiku Bayern Munich au Werder Bremen na kutawazwa bingwa, lakini iliteleza mara nyingi mechi ya mwisho.Hii ilitokea msimu uliopita pale Stuttgart ilipotoka nyuma na kutoroka na taji.

FC Schalke ilinyakua taji lake la mwisho la ubingwa wa Ujerumani 1958 hata kabla kuanzishwa kwa Bundesliga,1963.

Tangu kuanzishwa kwa Bundesliga,1963 ilipotawazwa FC cologne, mabingwa wa kwanza,Schalke haikumudu kuvaa taji tena.Msimu wa 1965,Schalke ilimaliza msimu ikuburura mkia ikiwsa timu ya mwisho kunusurika kuteremshwa chini.

Ilivuka salama mwaka huo kwavile Bundesliga ilipanuliwa kutoka timu 16 na kufanywa timu 18.

Bahati kama hiyo haikuiangukia Schalke miaka iliofuatia.Ilipofichuka kashfa kubwa ya kulishia hongo,Schalke ilikua usoni kabisa.

Lakini, mwaka baada ya kashfa hiyo ya hongo,Schalke iliibuka na mafanikio:Ilinyakua kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani ilipoizaba Kaiserslauten mabao 5:0 .

Lakini kufuatia ushindi huo, mambo yakarudi kuiendea kombo Schalke 04.Kwani, mnamo miaka ya 1980 ,schalke iliteremshwa mara tatu daraja ya pili ya Bundesliga.Hatahivyo, mashabiki wake wakivinjari,waliimba na kudai Schalke haitazikwa:

Kwa mashabiki, ilikua muhimu sana kwamba Schalke hata katika daraja ya pili inaendelea kutamba.Kwani, mashabiki wakihisi Schalke ni kama dini kwao.

Mnamo miaka ya 1990,Schalke iliweza mwishoe, kujikomboa kutoka misukosuko yake tena tangu kispoti hata kiuchumi.Hivi sasa Schalke inacheza katika uwanja wa kisasa kabisa wa dimba ulimwenguni.

1997,schalke ilijipatia ushindi wake mkubwa kabisa katika historia yake:Ilishinda kombe la Ulaya la UEFA.iliilaza Inter Milan katika finali ya duru 2.Ushindi ulikuja kupitia mikwaju ya penalty katika uwanja wa san Siro,huko Itali.

Na hivi ndivyo mtangazaji alivyosimulia uwanjani:

„Na sasa inapigwa penalty muhimu sana.Anaeipiga ni Marc Wilmots.Baada ya kupigwa penalty hiyo matokeo ni mabao 3:1 na anaipüiga chini kwa chini katika kona ya kushoto.Schalke ni mabingwa wa Kombe la UEFA.“

Ufunguo wa ushindi wa schalke alikua mchezaji wao aitwae Olaf Thon-profesa-kama walivyomuita mashabiki.

Olaf Thorn asema:

„Tulikua kikundi kilichofahamiana.Na bila ya shaka kilikua na tabia isio ya kawaida ya ari ya ushindi.Ilikua timu iliofahamiana na kuonana.“

Asema Olaf Thon,mchezaji wa zamani wa Schalke na timu ya taifa ya Ujerumani.

Lakini, licha ya ushindi wa kombe la Ulaya,Schalke imeshindwa tangu kuanzishwa Bundesliga,1963 kuvaa taji la bundesliga.Na hii licha ya kulinyemelea sana.

Mara mbili imeibuka makamo-bingwa na msimu uliomalizika ilimaliza pia 2 nyuma ya mabingwa Stuttgart.

Mmoja wa mastadi wake wa kubwa wakati ikivuma alikua Stan Libuda,aliekua na chenga za ajabu.Kabla ya kufariki kwake aliulizwa ana ombi gani ?

Jibu lake:

„Ningeomba mwanangu wa kiume na mama yangu wabaki na afya njema,sina zaidi isipokuwa kuomba pia Schalke kutawazwa mabingwa wa Ujerumani.“

 • Tarehe 13.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbi
 • Tarehe 13.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbi