1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schalke 04 yamtia hofu Sir Alex Ferguson

Aboubakary Jumaa Liongo15 Aprili 2011

Mchanganyiko wa kandanda la Ujerumani na mshambuliaji Mhispania Raul Gonzalez huenda ukaitoa kijasho Manchester United na kocha wake Sir Alex Ferguson katika mchuano wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/10uU0
Wachezaji wa Schalke wakifanya mazoeziPicha: AP

Schalke huenda wakawa timu ya pembeni kwa jina tu, lakini United haijawahi kuipiku timu yoyote ya Ujerumani katika mechi nne za mikondo miwili kwa kivumbi kama hicho na hata wakabanduliwa mara mbili dhidi ya Real Madrid wakati Raul alipokuwa akiichezea.

Klabu ya Borussia Dortmund iliwabandua Manchester United katika nusu fainali ya kinyang'anyiro hicho mwaka wa 1997 na Bayer Leverkusen ikawazaba katika awamu hiyo hiyo mwaka 2002. United pia iliondolewa katika mechi za robo fainali na Bayern Munich mwaka wa 2001 na 2010.

Ralf Rangnick Trainer FC Schalke 04 Flash-Galerie
Ralf Rangnick: Kocha wa Schalke 04Picha: dapd

Raul kwa upande wake alifunga mabao manne kati ya rekodi ya mabao yake 71 ya ligi ya mabingwa wakati Real ilipowafurusha United katika robo fainali ya mwaka wa 2000 na 2003.

Sasa united watakabiliwa na Schalke tarehe 26 katika uga wa Veltins Arena na Mei 4 uwanjani Old Trafford.

Kama tu Leverkusen mnamo mwaka wa 2002 Schalke hawajulikani saana kwenye ulingo mkubwa licha ya kutwaa kombe la UEFA katika miaka ya nyuma ambapo Leverkusen ilinyakua mwaka wa 1988 nayo Schalke ikachukua mwaka wa 1997 na hawajawahi tena kufikia hapo katika ligi ya mabingw.

Lakini sasa Schalke wamepata umaarufu duniani kwa kuwasambaratisha mabingwa watetezi Inter Milan wa Italia. Kocha wa Manchester United Alex Ferguson alihudhuria mchuano wa marudiano wa Schalke dhidi ya Inter, ambapo timu hiyo ya Ujerumani iliwashinda kwa urahisi Inter kwa mabao 2-1 na kuongeza kwa yale ya kwanza 5-2.

Schalke wako katikati mwa jedwali la ligi ya Ujerumani bundesliga na wanaonekana kufufuka hasa baada ya kuwasili kwa Ralf Rangnick aliyechukua nafasi ya Felix Magath aliyetimuliwa. Schalke pia wana mlinda lango wa Ujerumani Manuel Neuer ambaye aliwahi kuhusishwa na uvumi wa kujiunga na Manchester United lakini anaonekana kuelekea Bayern Munich.

Wachezaji kama vile Alexander Baumjohann na Jose Manuel Jurado wana ujuzi murwa huku naye kiungo wa kati Joel Matip na mwenzake Kyriakos papadopoulos ambao wote wana umri wa miaka 19 walionekana kuwakabili zaidi nyota wa Inter Milan japo hata umri wapo kwa pamoja unashinda wka mwaka mmoja tu ule wa mchezaji wa United Ryan Giggs ambaye ana umri wa miaka 37.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA

Mhariri:Aboubakary Liongo