SARAJEVO : Watoto 5 wateketea na moto | Habari za Ulimwengu | DW | 23.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SARAJEVO : Watoto 5 wateketea na moto

Takriban watoto watano wameuwawa na wengine zaidi ya 12 kujeruhiwa wakati moto ulipozuka kwenye kituo cha mayatima katika mji mkuu wa Bosnia Sarajevo.

Polisi na askari wa kuzima moto wamesema kwamba moto huo ulizuka kwenye ghorofa ya tatu ya jengo hilo la mayatima na kusambaa haraka kwenye vyumba ambapo watoto walikuwa wamelala mapema hapo jana asubuhi.

Askari wa kuzima moto wamewaokowa zaidi ya watoto 20 na watoto kadhaa waliojeruhiwa wako kwenye hali mbaya.

Uchunguzi juu ya sababu za kuzuka kwa moto huo unaendelea kufanyika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com