1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO:Dikteta wa zamani nchini Chile, Pinochet, atolewa waranti wa kukamatwa

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyY

Jaji moja nchini Chile ametuma waranti wa kukamatwa aliokuwa rais wa nchi hiyo Augusto Pinochet baada ya kumfungulia mashtaka katika kesi inaojulikana kwa jina la Villa Grimaldi inaohusu kupotea kwa watu 36, matukio 23 ya mateso na mauaji ya mtu moja. Jaji Alesandro Solis, ametupilia mbali hoja za upande wa utetezi kwamba afya ya dikteta huyo wa Pinochet, mwenye umri wa miaka 90 sasa, ni mbaya kuweza kufikishwa mahakamani.

Maelfu kadhaa ya raia walikamatwa wakati wa utawala wa Pinochet kwa tuhuma za makosa ya kisiasa.

Zaidi ya 3000 miongoni hao walitoweka na kiasi ya wengine 30,000 waliteswa gerezani kulingana na uchunguzi rasmi wa mwaka 2004.