1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Santiago Rais wa zamani wa Peru kurudishwa nyumbani kukabili mashitaka

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNs

Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori atapelekwa nyumbani kutoka Chile ili kujibu mashitaka ya rushwa na ukiukaji wa haki za binaadamu wakati wa utawala wake 1990 hadi 2000.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa mahakama kuu ya Chile hii leo Uamuzi huo hauwezi kubatilishwa na hivyo Fujimori atarudishwa nyumbani baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka saba. Bw Fujimori mwenye umri wa miaka 69 alikimbilia Japan mawaka 2000 kufuatia kashfa ya rushwa na akajiuzulu kwa barua aliyoituma kwa FAX akiwa hotelini mjini Tokyo. Wakili wa kiongozi huyo wa zamani Gabriel ZALIANSKI amesema mteja wake amekubaliana na uamuzi wa mahakama kupekwa Chile kujibu mashitaka yanayomkabili