Santa Cruz. Bolivia yataifa visima vya gesi na mafuta. | Habari za Ulimwengu | DW | 29.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Santa Cruz. Bolivia yataifa visima vya gesi na mafuta.

Serikali ya Bolivia imefikia makubaliano kuhusu nishati na makampuni 10 ya kigeni kabla ya muda wa mwisho kufika kwa makampuni ya kigeni kuingia mikataba ama kuondoka nchini humo.

Rais Evo Morales ametaifisha makampuni ya gesi na mafuta mwezi May kuipa serikali udhibiti zaidi pamoja na fedha zaidi.

Morales amesema hatua hiyo itaiingizia nchi hiyo dola bilioni nne kwa mwaka dhidi ya fedha zinazopatikana hivi sasa dola milioni 200 kwa mwaka.

Makampuni ya kigeni yatapaswa hivi sasa kufanyakazi

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com