1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA:Kiongozi mtoro wa al-Qaeda auliwa nchini Yemen

1 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD73

Majeshi ya usalama nchini Yemen yamemwuua kiongozi wa ngazi ya juu wa Alkaida aliekuwa anatafutwa baada ya kutoroka jela mapema mwaka huu.

Maafisa wa majeshi hayo wamesema kuwa kiongozi huyo Fawaz al Rabihi alihukumiwa adhabu ya kifo mwaka jana baada ya ,kupatikana na hatia ya kula njama za kuishambulia meli ya mafuta ya Ufaransa kwa kutumia mashua iliyojazwa mabomu.

Fawaz al Rabihi aliuliwa wakati majeshi ya usalama ya Yemen yalipoivamia nyumba moja mjini Sanaa.