1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA : Shambulio lajeruhi 30 msikitini

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBx

Washambuliaji wasiojulikana wameushambulia msikiti kwa bomu la petroli nchini Yemen hapo jana na kujeruhi watu 30 wanane kati yao hali zao zikiwa mbaya.

Shirika la habari la taifa Saba limesema washambuliaji hao walishambulia wakati wa sala kuu ya Ijumaa kwenye msikiti ulioko katika jimbo la Amran kaskazini mwa mji mkuu wa Sanaa.

Shirika hilo la habari limesema watu 30 wameunguwa moto na wanane wako kwenye hali mbaya baada ya watu wasiojulikana kuingia kwenye msikiti huo na kuwarushia wauumini mafuta ya petroli na baadae kuwawasha moto.

Haikuweza kujulikana mara moja nani aliehusika na shambulio hilo au iwapo kuna uhusiano wowote ule na uasi wa miaka mitatu uliosababisha maafa miongoni mwa kabila la watu wachache la Zaidi katika milima ya kaskazini nchini Yemen.