1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAN DIEGO:Carlifornia yaendelea kuungua

24 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7D8

Wizara ya ulinzi ya Marekani inapeleka wanajeshi ili kupambana na maafa ya moto katika jimbo la Carlifornia.

Wizara hiyo pia inapeleka zana za kuzimia moto pamoja na mahitaji kwa ajili ya watu waliohamishwa kutoka kwenye nyumba zao.

Rais G. Bush anatarajiwa kuenda kwenye jimbo hilo ili kujionea madhara yaliyosababishwa na mioto kadhaa.

Habari zinasema nyumba zaidi ya alfu 1 na mia tatu zimeshateketea. Watu nusu milioni wamelazimika kuzihama nyumba zao ili kuepuka maafa ya moto.

Na watabiri wa hali ya hewa wamesema joto linatazamiwa kuongezeka sambamba na pepo kali.