1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAMARA:Urusi na Umoja wa Ulaya kuendeleza mazungumzo

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0u

Viongozi wa Urusi na Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuendelea na mdahalo jengevu baada ya mkutano wao mkuu licha ya kuwapo tofauti katika masuala kadhaa baina yao.

Mkutano huo uliofanyika katika mji wa Samara kusini mwa Urusi, uliibikwa na tofauti za kisiasa pamoja na mzozo unaotokana na hatua ya Urusi kuipiga mafuruku Poland kuingiza nyama nchini Urusi.

Ili kuondosha tofauti hizo Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambae ni rais wa sasa wa baraza la Umoja wa Ulaya ametoa mwito juu ya kuanza mara moja, mazungumzo juu ya kuleta mapatano ya ushirikiano baina ya Urusi na Umoja huo.

Akizungumza baada ya mkutano , rais Vladmir Putin alisema kuwa Urusi na Umoja wa Ulaya zimekubaliana juu ya kupanuza ushirikiano wa kiuchumi.

Hatahivyo rais Putin amezilaumu nchi fulani za Umoja wa Ulaya kwa alichoita ubinafsi wa kiuchumi.