1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAINT PETERSBURG:Waandamanaji wa upinzani washambuliwa

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9c

Polisi wa kupambana na ghasia waliwashambulia na kuwazuia waandamanaji mjini St Petersburg walipokuwa wakifanya maandamano ya amani.Maandamano hayo yanalenga kupinga uongozi wa Rais Vladimir Putin ikiwa ni siku moja baada ya waandamanaji wengine wengi kukamatwa mjini Moscow.

Yapata waandamanaji alfu 2 kutoka upande unaopinga serikali wa The Other Russia walikusanyika katikati ya mji wa pili kwa ukubwa wa Urusi kutoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi ulio huru mwaka ujao.Rais Putin anamaliza muhula wake mwaka 2008.Takriban majeshi 1500 ya usalama yalishika doria katika eneo hilo la mji ili kuwazuia waandamanaji hao.

Polisi waliwapiga na kuwazuia waandamanaji wote waliojaribu kuvuka maeneo yaliyotengwa wakati wakifumka.

Baadhi ya waliokamatwa ni Eduard Limonov mmoja wa kiongozi wa chama cha upinzani cha The Other Russia.Mapambano hayo kati ya polisi na waandamanaji yameingia siku yake ya pili.

Hali inazidi kuwa ya wasiwasi huku uchaguzi wa rais ukisubiriwa mwaka ujao.Kwa mujibu wa katiba Rais Putin analazimika kuondoka madarakani punde muhula wake ukimalizika.hata hivyo kiongozi huyo ana ushawishi mkubwa nchini mwake kwa kusababisha ukuaji mkubwa wa uchumi.