1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

safari za serikali za muungano Ujerumani mikoani na Taifa ?

13 Oktoba 2009

Serikali za mseto zaelekea wapi ?

https://p.dw.com/p/K57T
Mwenyekiti mpya wa SPD ?(Gabriel-kushoto)Picha: dpa

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, yametuwama mno juu ya mada za ndani na hasa: Juhudi za kuunda serikali ya muungano katika daraja ya Taifa na mikoa na athari zake kwa jicho la ahadi zilizotolewa kwa wapigakura wakati wa kampeni za uchaguzi.

"BILD-ZEITUNG" juu ya serikali kuu ya muungano Taifa mjini Berlin,Laandika:

"Chama cha FDP cha kiliberali,kimepunguza sauti yake: Kwani, kutawala serikalini ni tofauti na kuwa safu ya upinzani.Je, waliberali hao baadae watapinduka cnini ? Chama cha FDP hakiweza kuufumbia macho ukweli upungufu wa fedha katika hazina ya serikali.Msukosuko wa fedha uliozuka haukuwa siri ya serikali.Kwahivyo, mshirima mdogo katika serikali ya muungano na mshirika mkubwa (CDU/CSU) katika baadhi ya madai yake FDP kinabidi kuregeza kamba...."

Ama gazeti la "STUTTGARTER NACHRICHTEN" linachambua ahadi ya chama hicho cha FDP cha kuwapunguzia watu kodi.Laandika:

"Ahadi za uchaguzi za chama cha FDP zilikuaje ? Wafanyakzi na waajiri , wapate fedha safi zaidi kutoka pato jumla kabla kukatwa kodi.Sasa majadiliano ya kuunda serikali ya muungano kati ya vyama, yanaingia hatua ya maamuzi. Itadhihirika ,kitabakia nini mwishoni mwa wiki hii kutoka ahadi walizotoa.

Hivi sasa kuna ishara kwamba,viongozi wa vyama vitatu vinavyounda serikali ya mseto -Bw.Westerwelle,Seehöfer na Bibi Angela Merkel, wanavuta pumzi wakirejea nyuma kutoka ahadi mbali mbali walizotoa ."

Likigeukia juhudi nyengine za kuunda serikali ya muungano baada ya uchaguzi wa majuzi mara hii mkoani Brandenburg, gazeti la "WESTFÄLISCHE NACHRICHTEN" kutoka Münster laandika:

"Hata kabla ya shubiri ya kuunda serikali ya mseto ya rangi ya "bendera ya Jamaika " mkoani Saarland ( rangi nyeusi,manjano na kijani),kidonge kingine kichungu kumeza kujitokeza huko Potsdam....

Baada ya uchaguzi wa Bunge la shirikisho ambamo chama cha SPD kilipata pigo kali ,darasa la rangi za bendera nchini linachambuliwa upya.Miko iliokuwapo inatupwa pembeni.majaribio na washirika wapya yanafanywa na mikakati inatungwa ambayo baadae, ihakikishe wingi wa kutawala sio tu mikoani ,pengine hata kitaifa."

Gazeti la " Augsburger Allgemeine" laichambua muungano mwengine mkoani Saarland.Laandika:

"Ghafula , chama cha SPD kimejikuta kimeangushwa na kimezingirwa huko na chama cha CDU kilicho elemea kidogo shoto na kile cha mrengo wa shoto zaidi cha LINKE. SPD kinabidi sasa kufuma upya mtandao wake :nani wa kuundanacho serikali na kupata wingi wa kutawala?

Mwenyekiti mpya wa chama na Katibu wake Bw.Gabriel na Bibi Nahles, wanapaswa sasa kukifuma chama kwa mfumo ambao unaweza baadae kufunga ndoa na mojawapo wa vyama.Kwa hivi sasa, serikali ya muungano ya mfumo wa "bendera ya rangi za Jamaika" mkoani Saarland, ni jaribio la mkoa mdogo kabisa ambao pole pole, mfano huo utakuja kubadili sura ya vyama nchini."

Muandishi: Ramadhan Ali /DPA

Mhariri: Abdul-Rahman