Saddam Hussein Anyongwa | Habari za Ulimwengu | DW | 30.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Saddam Hussein Anyongwa

TAARIFA YA HABARI ZA ULIMWENGU 30-12-06 11.00

BAGHDAD:

Rais wa zamani wa Iraq,Saddam Hussein alinyongwa mapema asubuhi ya leo kwa hatia ya kuhusika na mauaji ya watu kiasi cha 150 katika mji wa Dujail,unaokaliwa zaidi na wairaqi wa madhehebu ya shiia,1982.Sadam aliaga dunia mara , Sami al Askari,aliarifu kuwa marehemu aliongozwa na walinzi wa kiiraqi waliovalia mavazi meusi.Alikuwa amefungwa.Saddam alionekana shuwari kabisa na wala hakutetemeka.Saddam akiwa na umri wa miaka 69.

Hapo kabla, hakimu wa Marekani alilikataa ombi la dakika za mwisho la mawakili wa Saddam kuzuwia kukabidhiwa Saddam Iraq kutoka mikono ya jeshi la Marekani.

Ilikuwa mapema wiki hii pale Mahkama ya Rufaa ilipothibitisha hukumu ya kuuwawa Saddam na kuamuru itekelezwe mnamo muda wa siku 30.Leo ni siku kuu ya Idd el hajj nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com