1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yakanusha kukiunga mkono kikundi cha waasi cha M23

16 Julai 2012

Tangu kuzuka kwa uasi mpya mashariki mwa Kongo, ukiendeshwa na kikundi cha M23,Serikali mjini Kinshasa na Umoja wa Mataifa zimekuwa zikiishutumu Rwanda kukiunga mkono kikundi hicho, shutuma ambazo Rwanda imezikanusha.

https://p.dw.com/p/15YZI
Umoja wa Mataifa waishutumu Rwanda kukiunga mkono kikundi cha M23
Umoja wa Mataifa waishutumu Rwanda kukiunga mkono kikundi cha M23

Mwishoni mwa juma wapiganaji 24 wa kikundi hicho ambao walidai ni raia wa Rwanda walijisalimisha kwenye jeshi la Umoja wa Mataifa na kuomba warudishwe nyumbani. Lakini mpakani, Rwanda ilikataa kuwapokea wapiganaji hao na kuwarudisha nyuma. Daniel Gakuba amezungumza kwa njia ya simu na waziri wa usalama wa ndani wa Rwanda, Fadhil Harerimana, na kwanza alimuuliza, kwa nini Rwanda iliwakataa wapiganaji hao waliojisalimisha.

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Danieli Gakuba

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman