1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto kutohudhuria vikao vyote vya ICC

Samia Othman16 Januari 2014

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya mjini The Hague Uholanzi imeamua kwamba Makamo wa Rais wa Kenya William Ruto hatohitajika kuwepo katika vikao vyake vyote vya kesi inayomkabili ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

https://p.dw.com/p/1ArYJ
William Ruto - Makamo wa rais wa Kenya
William Ruto - Makamo wa rais wa KenyaPicha: Michael Kooren/AFP/Getty Images

Kutokana na uamuzi huo Ruto atapaswa kuwepo wakati wa kusomewa hukumu, pale waathirika wanapotoa ushahidi wao na siku tano za mwanzo za kusikilizwa kesi yake. Kutoka Kenya Sudi Mnette amezungumza na Ojwang Agina, ambae ni mwanasheria na mchambuzi wa masuala ya ICC na kwanza alimuuliza anauzungumziaje uamuzi huo? Kuskiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi:Sudi Mnette

Mhariri:Yusuf Saumu