1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Russia -na mfereji wake wa mafuta-vinu vya kinuklia viendelee ?

10 Januari 2007

Mada hizo 2 zimechambuliwa na wahariri wa magezti ya Ujerumani hii leo tena kwa mapana na marefu.Ila kali za Kanzela Angela Merkel kwa Moscow zimepewa heko.

https://p.dw.com/p/CHU0

Tukianza na mada inayogonga vichwa vya habari wakati huu –kuzuwia Russia mafuta yake kutiririka kwenye maboma ya Ulaya ya magharibi,kitendo hicho kimezusha kero kati ya Umoja wa Ulaya na Russia.

Kwani, kanzela Angela Merkel,mwenmyekiti wa sasa wa UU,ameituhumu Russia, kuchukua hatua hiyo bila kushauriana na wenzake,imepoteza imani yao.

Gazeti la HANDELSBLATT linalo chapishwa Düsseldorf linasema kwamba, mwishoe,inadhihirika kana kwamba, Kanzela Merkel ameweza sasa kujikomboa kutoka kivuli alichofunikwa na mtangulizi wake Gerhard Schröder katika usuhuba na Russia.

Yadhihirika wakati sasa umepita pale rais Wladmir Putin wa Russia akivikwa kilemba cha mdemokrasi bila ya kuwa ameibadili Russia kuwa dola la kisheria .

Ila alizotoa Bibi Merkel kwa Moscow kwa kitendo chake ilichofanya bila mashauriano-yaani kufunga mfereji wake wa mafuta, zilistahiki.Kwani, ilivyofanya Russia ,kufunga mfereji wake wa mafuta ,mtu hamfanyii si jirani yake seuze Umoja wa Ulaya-lasema Handelsblatt kutoka Düsseldorf.

Gazeti la KIELER NACHRICHTEN linasema kuwa, tuhuma za Bibi Merkel zinapata uzito kwavile, kwa upande mmoja amezitoa akiwa mwenyekiti wa UU wakati huu na kwa upande mwengine, akiwa mwenyekiti wa kundi la G-8-kundi la nchi tajiri za kiviwanda-yaani ile klabu ambayo Russia inapigania mno kujiunga nayo.

Na hii ndio lugha ambayo yadhihirika rais Putin anayoielewa.Umefika wakati kwa Moscow kubainisha wazi wazi kwamba, gharama ya kuwa na usuhuba mwema na UU ni kuaminika tangu kisiasa hata kiuchumi.

Likitukamilishia mada hii, gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE kutoka Essen laandika:

“Kuwa imesadifu dikteta wa Belorussia, Lukaschenko amewafungua macho viongozi wa Ulaya kuwa katika sera za nishati wafikirie upya sera zao, ni kiroja cha mambo.

Mstuko huu mpya wa mafuta umekuja pia na dawa yake.Umeonesha jinsi nchi za viwanda za Ulaya ya magharibi, zinavyoweza kudhurika na sasa zitafute katika kikao chake kilichoitwa haraka dawa mjarabu.

Gazeti la MANNHEIMER MORGEN ZEITUNG linausia:

„Yule sasa atakaedai kuachana na mpango wa kuvifunga vinu vya nishati ya kinuklia,huyo anapendekeza suluhisho rahisi na ataka kuseleleza hali ilivyo sasa badala haraka kubadili miundo ya sasa ya nishati .

Kurefusha kwa muda mfupi kufanya kazi kwa vinu vya kinuklia vinavyozalisha nishati, yamkini kwa kinu kimoja kimoja ni busara, lakini ikiwa wanasiasa hawatawashinikiza wataalamu wa sayansi hadi 2019 kusaka njia nyengine madhubuti za nishata zenye soko,hakuna kitakacho badilika.“