ROME.Mswaada utakaowalinda wapenzi wa jinsia sawa wapitishwa | Habari za Ulimwengu | DW | 09.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROME.Mswaada utakaowalinda wapenzi wa jinsia sawa wapitishwa

Baraza la mawaziri la Italia limeidhinisha mswaada utakaowapa haki watu wa jinsia sawa wanaoishi pamoja.

Lakini wakati huo huo baraza hilo la mawaziri halikuruhusu ndoa za watu wa jinsia sawa.

Waziri wa usawa wa Italia Barbara Pollastrini amesema mswaada huo utawalinda watu hao juu ya haki zao za mirathi na afya.

Baraza la mawaziri limepitisha mswaada huo licha ya upinzani na lawama kutoka chama cha Christian Demokratik na kanisa katoliki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com